Matukio mbalimbali kwenye Maonyesho ya Biashara Maputo - Mozambique. Nchi mbalimbali Duniani zilishiriki ikiwemo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuleta bidhaa zao mbalimbali. Maonyesho hayo yalifunguliwa tarehe 27 Agosti, 2018 na kufungwa tarehe 2 Septemba, 2018.

  • Kutoka kulia ni Bw. Albert Phillipo (Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Idara ya Diaspora), kushoto kwake ni Mheshimiwa Balozi Luhwavi, kushoto kwa Balozi ni Bw. Nelson Nkini (Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Mozambique) akifuatiwa na Bw. Dominic Francis Haule (Katibu Mtendaji Decision Foundation) kutoka Tanzania wakisikiliza maelezo kutoka kwa mfanyabiashara kutoka Kampuni ya ECO ya Botswana (Kampuni ya kusindika nyama za kopo) wakati wa Maonyesho ya Biashara Maputo.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na bidhaa zao kwenye banda la bidhaa za Tanzania wakati wa Maonyesho ya Biashara Maputo.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa na Bw. Albert Phillipo kulia kwake na Bw. Nelson Nkini kushoto kwake wakizunguka kwenye mabanda mbalimbali ya bidhaa wakati wa Maonyesho ya Biashara Maputo.
  • Kutoka kulia ni Bw. Albert Phillipo, kushoto kwake ni Bi. Getrude A. Ngwe'shemi (Manager wa Biashara Tan - Trade), kushoto kwa Bi. Getrude ni Bw. Nelson Nkini akifuatiwa na Mheshimiwa Balozi Luhwavi wakiwa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na bidhaa zao kutoka Tanzania katika banda la bidhaa za Tanzania kwenye Maonyesho ya Biashara Maputo.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania wakiwa na bidhaa zao kutoka Tanzania kwenye banda la bidhaa za Tanzania wakati wa Maonyesho ya Biashara Maputo.