Matukio mbalimbali kwenye Maonyesho ya Biashara za Tanzania na Mozambique yaliyofanyika Nampula. Maonyesho yalifunguliwa tarehe 20 Agosti, 2018 na kufungwa tarehe 25 Agosti, 2018

Lengo la Maonyesho hayo ni kujenga na kukuza mahusiano na ushirikiano wa raia wa Nchi zetu mbili za Tanzania na Mozambique katika kujenga, kukuza na kuimarisha Uchumi ambao ni nyenzo muhimu sana katika kuimarisha mahusiano ya raia wetu yaliyojengwa kipindi kirefu na waasisi wa Mataifa yetu mawili, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Samora Moses Machel.

  • Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akitoa maelezo juu ya bidhaa zinazozalishwa katika Jimbo la Nampula, kushoto kwa Mheshimiwa Gavana ni Mheshimiwa Balozi Rajabu Omari Luhwavi na kulia kwa Gavana ni Mkurugenzi wa viwanda na biashara Nampula Bw. Norberto Joao na wengine wakati wa Maonyesho ya biashara Nampula.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi na Gavana wa Nampula Mheshimiwa Victor Borges wakionja Juice ya viazi vitamu vinavyozalishwa Jimboni Nampula. Wakiwa na Bw. Bahima Mwinyi (Kaimu Mkuu Utawala) pembeni na wengine kwenye maonyesho ya Biashara Nampula.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akisalimiana na Bi. Brenda Mulenga wa Kampuni ya Darsh Industries inayohusika na usindikaji wa matunda na mbogamboga kutoka Tanzania, kulia kwa Balozi ni Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges na kushoto kwa Balozi ni Bw. Ali Abdallah Mohamed, Mtanzania anayemiliki Kiwanda cha kukoboa unga wa mahindi cha Super Chima kilichopo Nampula.
  • Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akipata maelezo kutoka kwa Bi. Brenda Mulenga kuhusu bidhaa zinazozalishwa Tanzania kwenye Kampuni ya Darsh Industries inayohusika na usindikaji wa matunda na mbogamboga. Kushoto kwa Gavana ni Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi, kushoto kwa Balozi ni Bw. Ali Abdallah Mohamed, Mtanzania anayemiliki Kiwanda cha kukoboa unga wa mahindi cha Super Chima kilichopo Nampula wakiwa kwenye Maonyesho ya Biashara Nampula.
  • Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akipata maelezo kutoka kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania kuhusu bidhaa za nguo kutoka Tanzania. Kushoto kwa Gavana ni Mheshimiwa Balozi Luhwavi na kushoto kwa Balozi ni Bw. Bahima Mwinyi (Kaimu Mkuu Utawala) wakiwa kwenye Maonyesho ya Biashara Nampula.
  • Mheshimiwa Balozi Rajabu Omari Luhwavi akitoa maelezo ya shukrani kwa uongozi wa Jimbo la Nampula kwa kuwapokea Wafanyabiashara wa Tanzania na kwa kuwa tayari kufanya Maonyesho pamoja.
  • Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Viwanda na Biashara Bw. Norberto Joao, kulia kwake ni Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akifuatiwa na Mheshimiwa Balozi Luhwavi, kulia kwa Balozi ni Mkuu wa Wilaya ya Nampula Bw. Alfredo Matata wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Biashara Nampula.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akibadilishana mawazo na Gavana wa Nampula Mheshimiwa Victor Borges, pembeni yao ni Bw. Bahima Mwinyi (Kaimu Mkuu Utawala) wakati wa Maonyesho ya Biashara Nampula.