Rais Nyusi na Serikali yake ya Chama cha Frelimo jana ziliwezesha kusainiwa kwa Mkataba wa kusalimisha silaha kutoka kwa wapiganaji wa lililokuwa kundi la Waasi la Renamo ambalo baadae lilijibadilisha na kuwa chama cha Siasa dhidi ya chama Tawala cha Frelimo.

  • Mheshimiwa Jacinto Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Mozambique na Bwana Ossofo Momade kiongozi wa kundi la Waasi Renamo wakikabidhiana Mkataba walio usaini wa kusalimisha silaha kutoka kwa wapiganaji wa Renamo.
  • Mheshimiwa Nyusi akikumbatiana na kiongozi wa Renamo Bwana Ossofo Momade baada ya kusaini mkataba wa kusalimisha silaha kutoka kwa wapiganaji wa Renamo.