MAPUTO, JULAI 25, 2020 - Rais wa Serikali wa Jamhuri Msumbiji , Filipe Jacinto Nyusi, ametuma Salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mh. John Pombe Magufuli, kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa nchi ya Tanzania, Benjamin William Mkapa, ambae amefariki tarehe 24 ya mwezi Julai 2020, baada ya kuugua.

Katika ujumbe huo, Rais Nyusi alisema kuwa ni huzuni kubwa sana ya kuondokewa na Rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kwa niaba ya watu, Serikali ya Jamhuri ya Msumbiji na kwa niaba yangu binafsi ningependa kuwaambia, Wananchi na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tunayo huzuni kubwa ndani ya mioyo yetu, kwa familia iliyofiwa, tunatuma salamu za pole na tunaahidi mshikamano kwenye hili na tunaimani Mwenyezi Mungu atawapatia nguvu kwenye wakati huu wa huzuni kwa kufiwa na mpendwa wenu, ”inasomeka hivyo kwenye ujumbe kutoka kwa Rais Nyusi.

Rais Mkapa alikuwa ni mzalendo wa kweli na mwasisi wa Afrika, aliyetumikia nchi yake kama mwanadiplomasia mwenye ujuzi na Kiongozi ambaye aliongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka kumi, kwa nia ya kuleta  utulivu wa kisiasa kupitia mfumo wa vyama vyingi akiwa na lengo la kuweka misingi bora zaidi kwa maendeleo  ya uchumi.

"Tutamkukumbuka kama mshindi wa kukuza mahusiano ya ndani ya kisiasa na kijamii katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Bara la Afrika. Rais Mkapa alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha uhusiano bora wa undugu, urafiki, mshikamano na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji, ndio maana yeye ni rafiki wa kweli wa watu wa Msumbiji ", amesema Rais Nyusi.