1.0 UTANGULIZI:

Ubalozi ulipata mwaliko kutoka Tantrade wa kuziarifu chi tunazoziwakilisha kushiriki maonyesho ya kimataifa yatakayofanyika Dar es salaam, barabara ya kilwa, Sabasaba, mwezi Julai mwaka 2019. Katika mwaliko huo Tantrade waliomba Ubalozi uhamasishe pia wafanyabiashara toka kwenye maeneo yetu ya uwakilishi kushiriki maonyesho hayo. Uhamasishaji huo uhusishe watanzania wafanyabiashara waishio kwenye maeneo ya uwakilishi na wale wenyeji (wafanyabiashara wazawa) kwenye maeneo ya uwakilishi. Kwa kuzingatia hitaji hilo, Mheshimiwa Balozi aliamua kwenda Jimboni Nampula kukutana na makundi ya wafanyabiashara kutoka katika kundi:

I. Wafanyabiashara Watanzania waishio Jimboni humo na maeneo ya jirani ya Jimbo la Nampula.

II. Wafanyabiashara wenyeji katika Jimbo la Nampula.

1.1 MAZUNGUMZO BAINA YA MHE. BALOZI NA JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO NAMPULA.

Mheshimiwa Balozi alikutana na uongozi wa jumuiya ya watanzania waishio Jimboni Nampula. Mheshimiwa Balozi aliwashukuru kwa muitikio wao na kueleza ujio wake ni kuzungumzia juu ya mabo mawili ambayo ni:

i) Maandalizi ya kushiriki maonyesho ya kimataifa yanayotarajiwa kufanyika mwezi Julai jijini Dar es Salaam.

ii) Kujadili juu ya maonyesho ya Bidhaa za kitanzania hapa Jimboni Nampula wakati wowote mwezi Agosti,2019 kama ilivyofanyika mwaka jana.

Mheshimiwa Balozi alieleza tumepokea mwaliko kutoka Tantrade na kwamba Ubalozi unao wajibu wa kuja kuwaeleza hasa viongozi wa Jumuiya ya watanzania kuhamasisha wafanyabiashara wote waishio Nampula na maeneo jirani kushiriki maonyesho ya Sabasaba ambayo yamepangwa kufanyika mwezi Julai, 2019. Hivyo, Ubalozi ukishirikiana na viongozi wa Jumuiya unapaswa kujadili namna gani washiriki wanaweza kushiriki maonyesho hayo kwani lazima kutakuwa na gharama ya ushiriki kwenda, malazi na kurudi Nampula. Washiriki (Viongozi wa Jumuiya) walishauri ni vizuri ziara hiyo ihusishe pia washiriki kwenda kutembelea mbuga zetu za wanyama, kwani kwa kufanya hivyo tutakua tumetangaza pia utalii wa mbuga zetu za wanyama. Hivyo basi, gharama hizi zihusishe nauli, malazi na gharama za usafiri wa ndani nchini Tanzania. Mheshimiwa Balozi aliwaomba viongozi hao wajadiliane ni kiasi gani wanashiriki wachangie. Baada ya majadiliano viongozi hao walikubaliana kila mshiriki atoe kiasi cha Dola za Kimarekani (USD 500) ambazo zitaweza kuhudumia gharama zote isipokuwa Chakula kwani waliona ni vyema kila mshiriki ajigharamie chakula kwakua chakula ni utashi wa kila mshiriki. Aidha, katika mazungumzo haya, ilikubaliwa kwamba siku inayofuata tarehe 18 Aprili,2019 kuitishwe mkutano wa wafanyabiashara wote waliopo Nampula pia mkutano huo ushirikishe taasisi ya viwanda na biashara ya Jimbo, Taasisi ya Sekta binafsi (CTA), Taasisi inayohusika na uwekezaji (APIEX) pamoja na jumuiya zote za wafanyabiashara.

1.2 MKUTANO WA WAFANYABIASHARA WOTE WAISHIO NAMPULA NA TAASISI ZOTE ZA KIBIASHARA

Tarehe 18 April,2019 Mheshimiwa Balozi alikutana na wafanyabiashara wote washio Jimboni Nampula kwa kuanza, Mheshimiwa Balozi aliwashukuru kwa kujitokeza kwa wingi (Mahudhurio yao yameambatanishwa), ikumbukwe Ubalozi wa Tanzania nchini Mozambique umedhamiria kuiunganisha Mozambique hasa eneo hili la kaskazini na Tanzania katika kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, kwa kuzingatia hilo, mwezi Agosti mwaka jana, Ubalozi ulileta wafanyabiashara wa kitanzania ambao walikuja kushiriki maonyesho ambayo yaliandaliwa na Ubalozi kwa kushirikiana na uongozi wa ofisi ya Gavana wa Jimbo la Nampula. Ubalozi uliwasilisha taarifa kwamba Serikali ya Tanzania kupitia taasisi yake ya TAN-TRADE imeandaa maonyesho ya kimataifa yatakayofanyika mwezi Julai 2019, Jijini Dar es salaam, wafanyabiashara waishio Nampula na maeneo mengine ya kaskazini wakatumia fursa hii kwenda kutangaza biashara zao na kujifunza ili kupata masoko ya biashara zao. Hivyo basi, Ubalozi kwa kushirikiana na Jumuiya ya Watanzania walishiriki, hata hivyo ili zoezi hili liweze kufanikiwa zipo gharama za ushiriki ambapo kila mshiriki atalazimika kuchangia, gharama hizo ambazo zitahusisha Nauli, malazi na chakula. Baada ya majadiliano hayo, washiriki walikubaliana kila mshiriki atachangia kiasi cha USD 600 ambazo zitatumika kama nauli, malazi, chakula na usafiri wa ndani. Ili zoezi liweze kufanikiwa, wajumbe walikubaliana kuunda kamati ndogo itakayoratibu uhamasishaji na ukusanyaji michango. Kamati hiyo itakuwa na watu wafuatao:

JINA KAMILI                                                                 TAASISI ANAYOTOKEA

1. Juliana Harculette                                                      CTA

2. Fransisca Dagdo                                                       Viwanda na Biashara

3. Ali Abdula                                                                  Jumuiya ya Watanzania

4. Anko Machano                                                          Jumuiya ya Watanzania

5. Saidi Ali                                                                     Mwakilishi wa Wafanyabiashara Wadogo

6. Jemian Mapuazi                                                         Mkalimani

7. Nobert                                                                       Mkurugenzi - Viwanda na Biashara

8. Mwenyekiti - CTA                                                      CTA Jimbo la Nampula                                                             

Kazi ya kamati hiyo itakuwa ni kuhamasisha na kufanya tathmini juu ya mwenendo wa maandalizi yanavyokwenda na kuwasiliana na Ubalozi. Washirika wote walikubaliana kwa pamoja na wakakubaliana ili kurahisisha mawasiliano kutaundwa kundi(group) la whatsapp ambalo taarifa zote na maswali au ufafanuzi utakuwa unaulizwa na kutolewa pale.

Mwisho, Mheshimiwa Balozi aliwashukuru wajumbe kwa mwitiko wao na ana matumaini makubwa kwamba kamati iliyoteuliwa itafanikisha vyema ziara hiyo.

Nawasilisha.