Uzinduzi wa ofisi ya E-Commerce and Trade nchini Eswatini ambayo ilianzishwa na African Continental Free Trade Area (AFCFTA). Ilizinduliwa na African Union chiniya programu ya African Electronic group. Mkutano huo ulifanyika tarehe 4 Oktoba, 2019. lengo lake ni kufungua E-Commerce kwa soko la kibiashara kwa kanda ya kusini mwa Afrika. Uzinduzi wa programu hiyo ulifanywa na Mfalme Mswati wa III ambapo Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia.

Wawakilishi wa Tume ya Umoja wa Afrika, Wakurugenzi wa E-Trade group na wawakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ikiwa ni utekelezaji wa maadhimio ya kikao cha umoja wa Afrika kilichofanyika Niamey Mji Mkuu wa NIGER. Lengo ni kukuza biashara ya E-Trade Commerce kufikia asilimia 77 katika kipindi cha miaka mitatu.

Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara walialikwa kuhudhuria mkutano huu lakini kutokana na majukumu mengine ya kitaifa, Mhe. Rais Magufuli alimteua Mhe. Balozi Rajabu Luhwavi kumuwakilisha katika Mkutano huo.

  • Kutoka kulia ni Waziri wa Biashara, kushoto kwake ni Waziri wa Fedha, kushoto kwa Waziri wa Fedha ni Naibu Waziri Mkuu, kushoto kwake ni Balozi wa Malawi, akifuatiwa na mwakilishi kutoka Serikali ya Lesotho akifuatiwa na Balozi Rajabu Luhwavi walipohudhuria uzinduzi wa Ofisi ya E-Commerce and Trade nchini Eswatini.