Ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Balozi nchini Madagascar ilifanyika kuanzia tarehe 11 - 16 Novemba, 2019. Katika ziara hiyo Mheshimiwa Balozi aliambatana na Mwambata Jeshi na Mkurugenzi Mkuu (CEO) Taufiq Salim Turky mfanya biashara wa Kitanzania wa kampuni ya VIGOR TURKYS GROUP. Lengo kuu la ziara hiyo ni kutafuta fursa za uwekezaji na kufanya biashara kwa Wafanyabiashara wa Tanzania katika Jamhuri ya Madagascar.

Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ulipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Maliasili, Uchukuzi na Hali ya Hewa, Waziri wa Viwanda, Biashara na Kazi za Mikono, Waziri wa Uchumi na Fedha, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje. Pamoja na mazungumzo hayo, Ujumbe ulipata fursa ya kutembelea Mji wa Antsirabe uliopo km 171 toka Jiji la Antananarivo na Kiwanda cha nguo kinachoshona mavazi ya michezo mbalimbali (Sports Wear).

  • Kutoka kulia ni Mheshiomiwa Balozi Luhwavi, kushoto kwake ni Waziri wa Uchumi na Fedha Mheshimiwa Richard Randriamandranto, kushoto kwa Waziri ni Mr. Toufiq Salim Turky, mwekezaji kutoka Tanzania anawakilisha Kampuni ya Vigor Turkys Group.
  • Kutoka kushoto ni Balozi Luhwavi, kulia kwake ni Waziri wa Maliasili, Uchukuzi na Hali ya Hewa Mhe. Joel Randriamandranto. Kulia kwa Waziri ni Mr. Toufiq Salim Turky, Mwekezaji kutoka Tanzania anawakilisha Kampuni ya Vigor Turkys Group.
  • Mheshimiwa Balozi Luhwavi akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Tahirimiakadaza Ratsimandao baada ya mazungumzo na Balozi alipotoa shukrani ya maandalio ya Ziara hiyo yaliyofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje. Kulia kwa Waziri ni Mr. Toufiq Salim Turky, Mwekezaji kutoka Tanzania anawakilisha Kampuni ya Vigor Turkys Group.